Waliosambaza Video Chafu, za Denti Chuo Kikuu, Jela Miaka 3…



‘CONNECTION’ ndiyo msemo unaotrend (sambaa) kila kona ya jiji la Dar, baada ya video chafu ya mwanadada mmoja anayedaiwa kuwa ni denti wa Chuo Kikuu (jina linafi chwa) jijini Dar es Salaam, kuvujishwa na marafi ki zake.


 


Kufuatia kuvuja kwa video hiyo chafu, kila mtu anaomba kutumiwa video hiyo na kisha naye kuisambaza, jambo ambalo Jeshi la Polisi nchini, limeonya kuwa mkono wa sheria utafuata dhidi yao. Tukio hilo limesababisha kuibuka kwa taarifa mbalimbali huku mhanga wa video hiyo akidaiwa kunywa sumu na kufariki dunia.


 


TUKIO LILIVYOANZA


Tukio hilo lilianza kusambaa kama moto wa kifuu juzi jioni, huku kila mmoja akieleza chanzo chake, lakini kwa mujibu wa rafi ki wa karibu (shogaye) wa mlimbwende huyo ambaye alijitambulisha kuwa wanasoma wote katika chuo hicho, alimwaga mkanda mzima na kudai kuwa, shoga yake huyo hajafariki.


 


“Huyu dada anasoma chuo kikuu cha (anakitaja), alikuwa na mpenzi wake ambaye kwa sasa wameshaachana. Kipindi wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi, huyo jamaa alikuwa anamwambia huyo dada amtumie picha na video zake akiwa mtupu.


 


“Basi tena kama unavyojua wanawake sijui nani katuloga, Shoga yangu akawa anatuma kweli hizo video na zingine wakawa wanarekodi kabisa wakiwa pamoja, mwisho wa siku wakaachana, ndipo inasemekana huyo, mwanaume akaanza kuvujisha hizo video,” alisema mwanadada huyo aliyeomba jina lake kuhifadhiwa.


 


Mbali na chanzo hicho, chanzo kingine kinadai video hizo alivujisha rafi ki yake aliyekuwa amemuachia simu yake.


 


“Inasemekana hizo video na simu yake, alimuachia rafi ki yake amuwekee chaji yeye anaenda kusoma na wenziye, ndipo mwisho wa siku huyo rafi ki yake akaanza kuipekuapekua hadi kukutana na video hizo ambapo akaanza kujitumia na kuzisambaza kwa wengine,” kilisema chanzo hicho.


 


POLISI WAFUNGUKA


Aidha, kutokana na hali hiyo, Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha uhalifu wa kimtandao kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Joshua Mwangasa, alikiri kutambua uwepo wa taarifa za tukio hilo la video za utupu kuvujishwa.


 


Licha ya kubainisha kuwa kitengo hicho kinaendelea kufuatilia tukio hilo, alikataa kuthibitisha taarifa za mhanga wa tukio hilo kujiua na kumtaka mwandishi azungumze na msemaji wa Jeshi la Polisi. Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime naye alithibitisha kuwepo kwa taarifa za tukio hilo na kumtaka mwandishi asubiri wakati akihakiki taarifa za mwanadada huyo kujiua.


 


KIBANO KIKALI


Aidha, Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salam, Lazaro Mambosasa alionya watu wanaoendelea kusambaza video hizo za tukio hilo.


 


“Kwa sababu kwa sheria inatamka wazi kuwa analiyevujisha, na anayendelea kusambaza wote wana makosa, ukipoke video au picha za aina hiyo usisambaze, zifute, ukisambaza na wewe unaingia kwenye mkono wa sheria,” alisema.


 


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga alifafanua madhara ya watu wanaoendelea kusambaza video hizo na kuonya kuwa, sheria inaweza kuwabana.


 


“Kwa sababu kwa mujibu wa sheria ya makosa mtandaoni ya mwaka 2015, kifungu cha 23 kinabainisha wazi kuwa, wanaosambaza video hizo chafu, wanaweza kukumbana na adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela, faini shilingi milioni tano au vyote kwa pamoja.


 


“Hili ni jambo ambalo hakika watu hawatakiwi kulifurahia na kuona kama ni shangwe kila mmoja kutaka kuona na kumrushia mwenzake, kwa hiyo inabidi tuwe makini sana na hizi video chafu,” alisema Henga.


Hata hivyo, mwanaharakati huyo wa haki za binadamu, aliwaonya wanawake kutoendelea kukubali kudhalilishwa kingono kama kujipiga picha na video za utupu kwa kuwa ni jambo linalotweza utu wao.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad