Shule ya sekondari ya St Mark’s iliyopo Kongowe, Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, imeandaa mkakati wa kuwatambua wanafunzi walio chini kiuwezo na kuwasaidia ili nao waweze kufanya vizuri katika masomo yao.
Akizungumza wakati wa mahafali ya kidato cha nne mwalimu mkuu wa shule hiyo, Leticia Joseph amesema.
“Tunatambua baadhi ya wanafunzi wanakuwa chini kiuwezo darasani baada ya kubaini hilo shule imeandaa mkakati ambapo wanafunzi wasio na uwezo wanatambuliwa na kusaidiwa ili waweze kuinuka kielimu,”amesema.
Ameendelea kusema kuwa shule yao imekuwa na mafanikio makubwa katika ufaulu na hali hiyo kuifanya shule hiyo kuwa na matokeo mazuri kila mwaka ambapo kidato cha nne katika mitihani ya mwisho wanafaulu na kujiunga na kidato cha tano na wengine kujiunga vyuo.
“Mafanikio haya yanatokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya walimu na wanafunzi katika masomo yanayotolewa na mafanikio mengine ambayo shule imekuwa ikiyapata kutokana na kufanya mitihani vizuri ni uwepo wa walimu wa wa kutosha, maabara zenye vifaa vya kutosha, maktaba yenye vifaa vya kujifunzia.
“Shule imewalea kimaadili wanafunzi hivyo mkitoka shule mkirudi nyumbani msijiingize katika Mambo yasiyofaa mnatakiwa kuyaendeleza yale mliyoyapata shuleni.” alimaliza kusema.