Kufuatia malalamiko ya Watanzania kudhulumiwa wanapojaribu kununua magari mtandaoni, kutotumiwa kwa wakati na kutumiwa magari yasiyo na sifa, Ubalozi wa Tanzania nchini Japan umewataka wafanye uchunguzi kabla ya kutuma fedha
Umesema ni vigumu kwa fedha ambazo imeshatumwa kurejeshwa kutokana na Sheria za nchini humo kwakuwa Mamlaka huanzisha shauri dhidi ya mtu/kampuni iliyokiuka mkataba na sio ankara za malipo ambazo wengi huwa nazo
Aidha, Watanzania wanaoagiza magari wametakiwa kuangalia tovuti zaidi ya moja wanapotaka kufanya hivyo ili kufahamu bei za wastani za magari