SALVATORY NTANDU
Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka Nchini (DPP) Biswalo Mganga amewafutia Mashtaka na kuagiza kuachiwa kuwachia huru Mahabusu 147 katika mkoa wa Shinyanga ambao walikuwa wakisubiri kesi zao kutajwa Mahakamani na kuwataka kuwa raia wema katika maeneo wanayoishi sambamba na kutojihusisha na vitendo vya uhalifu.
Akizungumza Septemba 3,20202 Mjini Kahama katika Hafla maalumu ya uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ya Wilaya hiyo Biswalo amesema wamezingatia vigezo vikuu viwili vikuu vinavyotakiwa na kwa mujibu wa sheria ambavyo ni pamoja na kuzingatia Maslahi ya taifa na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha katika mashauri hayo.
“Wengine tumewafutia mashitaka kutokana ushahidi uliopo katika mashauri yao kutojitosheleza ambao utawezesha kuwatia hatiani pasipo kuacha shaka yeyote,pamoja na kuangalia maslahi ya taifa katika uendeshaji wa kesi hizo,”alisema Mganga.
Alisema kuwa miongoni makosa yaliyofutwa kwa mahabusu hao ni pamoja na Mauaji,kupigana,kukamatwa na gongo,na kuingia kwa Jinai(Uvamizi wa migodi bila ya kuwa na vibali) ambayo yalikuwa bado hayajatolewa maamuzi.
Awali akitoa Taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi ya Mashitaka ya Mkoa wa Shinyanga Naibu Msajili wa Mahakama kuu Kanda ya shinyanga alisema kuwa wilaya ya kahama yenye Halmashauri tatu za Msalala,Ushetu na Kahama Mjini zinamatukio mengi ya Uhalifu ikilinganishwa na maeneo mengine mkoani humo.
“Wastani wa Mshauri mbalimbali ya Jinai yanayofunguliwa katika ofisi yetu ya mkoa kwa mwaka kutoka kahama ni 1300 ndio maana tumelazimika kuongeza Mahakimu wawili ili kuhakikisha wanasikiliza mashauri hayo kwa wakati hivyo kufunguliwa kwa ofisi hiyo kutasaidia kupunguza msongamano wa wafungwa katika Gereza la kahama,”alisema Mbuya.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amoni Mpanju alisema kuwa katika ziara waliotembelea Magereza katika Mikoa ya Shinyanga na Geita washitakiwa wengi ni wa makosa ya mauaji yatokanayo na Ramli chonganishi yatokanayo na migogoro ya kifamilia.
“Inasikitisha kwa karine hii bado kunawatu wanaimani za kishirikina serikali itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu watakaobainika kufanya shughuli za ramli chinganishi sambamba na wanaotekeleza mauaji hayo,”alisema Mpanju.
Sambamba na hilo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria Mpanju amewaagiza wakurugenzi wote nchini kuhakikisha kila wanapojenga majengo ya Umma kutenga vyumba viwili kwaajili ya Ofisi ya Taifa ya Mashitaka ili kurahisisha utendaji kazi na utoaji wa haki kwa wananchi.