Watu 22 Wamepoteza Maisha Katika Ajali ya Ndege ya Kijeshi Kharkiv nchini Ukraine

 




Kulingana na ripoti za awali, watu 22 wamepoteza maisha katika ajali ya ndege ya kijeshi, Kharkiv nchini Ukraine.

Katika taarifa iliyotolewa na Huduma ya Dharura ya UKraine, imeripotiwa kuwa ndege aina ya AN-26 ya jeshi la Ukraine imeanguka karibu na uwanja wa ndege wa kijeshi katika mji wa Kharkov.


Katika taarifa hiyo, iliyoeleza kuwa watu 28 walikuwa kwenye ndege hiyo, imebainishwa kuwa watu 22 wamefariki, watu 2 wamejeruhiwa na watu 4 wanatafutwa.


Imerekodiwa kuwa huduma za dharura zimetumwa katika eneo la tukio.


Imeripotiwa kuwa Rais Vladimir Zelensky atafika  eneo hilo leo.


Kwa upande mwingine, Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu ametuma ujumbe wa pole kwa Ukraine.


Çavuşoğlu, katika taarifa kwenye ukurasa wake wa Twitter, ameandika,


"Ninaelewa maumivu ya familia za wale waliopoteza maisha katika ajali mjini Kharkiv nchini Ukraine, na ninatoa pole kwa ndugu na marafiki wa Ukraine."


Ujumbe wa Çavuşoğlu umejibiwa kwenye akaunti ya Twitter ya Ubalozi wa Ukraine huko Ankara,


"Asante Uturuki, rafiki yetu.", ulisema ujumbe huo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad