Waumini Wamzomea Mchungaji kwa Kuwashurutisha Kulipa Fungu la Kumi



Mchungaji wa kanisa moja mtaani Huruma, Nairobi aliwaudhi waumini baada ya kutishia kuwa atafunga kanisa sababu hawatoi fungu la kumi.


Duru zinaarifu kwamba wakati wa tangazo hilo. Pasta alikuwa amehuzunika mno akidai waumini wa kanisa hilo wamekuwa vichwa ngumu na kwamba hawakuwa waaminifu tena.


Waumini wamzomea mchungaji kwa kuwashurutisha kudai fungu la kumi

Picha ya waumini wakiabudu kanisani. Picha: UGC.

Kulingana na Taifa Leo, pasta aliwasuta vikali kwa kupenda kuhudhuria ibada mikono mitupu bila kutoa sadaka na fungu la kumi vizuri.


“Hili kanisa nilianzisha mimi nikiwa na mke wangu. Nimekuwa nikiwaombea kila siku lakini naona mmekuwa wakaidi,”


“Mmekuwa mkija hapa lakini hamtoi sadaka ya kutosha. Isitoshe, fungu la kumi pia hamtoi. Mnataka niishi vipi,” pasta aliwaka.


Penyenye zinaarifu kwamba waumini walibaki midomo wazi wakimwangalia pasta akiwafokea.


“Mimi sitawavumilia. Mtindo ukiwa ni huu, basi sina budi ila kulifunga kanisa na kuenda kulifungua kwingine,” alisema mchungaji.


Semi za pasta ziliwasha moto kanisani na kwa hasira waumini wakanyanyuka vitini wakaanza kumzomea vikali kwa kufungua kanisa akinuia kujitajirisha kutoka mifuko ya watu.


Waumini wamzomea mchungaji kwa kuwashurutisha kulipa fungu la kumi

Picha ya kanisa.

“Hatukujua kanisa hili ni mali yako. Hatukuja hapa kutoa hela bali kumuabudu Mungu. Kaa hapo na kanisa lako. Fungu la kumi hatutoi,” waumini walisema huku wakiondoka kanisani mmoja baada ya mwingine.


Hata hivyo semasema zinaarifu kuwa matamshi ya waumini hayakumguza pasta.


“Hamnitishi nyinyi. Mwanzo hamna hata asante kabisa. Endeni kabisa, wengine watakuja tu,” pasta aliwafokea.


Kwingineko waumini katika mtandao wa kijamii walizusha vikali baada ya pasta wa kanisa moja mtaani Pipeline kuwazuia kufuatailia ibada kwa sababu hawajatoa sadaka.


Inasemekana pasta alifungua mtandao ambao amekuwa akiwatumia kondoo wake ambao hawawezi fika kanisani mahubiri.


Waumini walifurahia sana hatua ya pasta hata wakampongeza wakisema alifanya jambo la maana kuhakikisha injili inasonga mbele.

Duru zinaairifu kwamba mchungaji aliwarai kuwa waaminifu na kuendelea kutoa sadaka zao kwa minajili ya kuendeleza ibada.

Hata hivyo, wengi wao walisalia kimya na kulalamika kwamba kutokana na hali ngumu ya maisha haingekuwa rahisi kwao kutoa sadaka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad