Yanga bado hawana timu – Mchambuzi, Edo Kumwembe



Mchambuzi nguli wa mchezo wa soka nchini, Edo Kumwembe amekichambua kikosi cha Yang SC baada ya kupata sare ya goli 1 – 1 mbele ya TZ Prisons katika mechi yao ya kwanza kwenye msimu huu mpya wa 2020/21 uliyoanza kutimua vumbi hapo jana siku ya Jumapili.




Edo ambaye ni mahiri kwenye uchambuzi wa mpira wa miguu amesema kuwa Yanga kwa mchezaji mmoja mmoja wapo vizuri, lakini unaona kabisa bado hawana timu.


”Yanga kwa mchezaji mmoja mmoja wapo vizuri, lakini unaona kabisa bado hawana timu, yani unaona kabisa bado hawana timu lakini mchezaji mmoja mmoja kila unayemgusa unaona hakuangushi saaana.”- Edo Kumwembe


Edo kupitia kipindi cha Sports Arena cha Wasafi Tv, ameongeza ”Watu wana m-target sana Nchimbi wakati mwingine na wanamtoa mchezoni, Ditram Nchimbi ndiyo aliyekuwa anaipa sana timu uhai.”


”Watu walifikiria nafasi ya Ditram na Kaseke wangeanza wachezaji wa kigeni, nafikiri kocha wa Yanga kama vile kawaambia nyie tazameni Ligi Kuu yetu inavyokuwa ile ilikuwa ni mechi yetu dhidi ya Burundi ya kirafiki lakini hii ndiyo Ligi Kuu inavyokuwa.”


”Akawaeka nje ingawa naambiwa Mukoko na Tuisila ati zao za uhamisho wa Kimataifa zilichelewa ndiyomaana wakakaa katika benchi. Lakini ukiangalia hata walio anza walikuwa na uwezo wa kuipa Yanga ushindi yule Sarpong Yanga wamepata ongezeko zuri kabisa anawazidi Molinga na Ykpe kwa maana ya kucheza mpira, anasifa zote za ushambuliaji.”


Mabingwa hao wa Kihistoria Ligi Kuu Tanzania Young Africans Sports Club hapo jana walitoka sare ya goli 1 -1 kwenye mchezo wao wa kwanza wa kufungua pazia la msimu 2020/21, katika mchezo huo goli la Yanga likifungwa na Saporng na lile la Prisons likiwekwa kimyani na Lambert Sabiyanka.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad