Yanga Waichapa Mtibwa Sugar Ligi Kuu



Yanga SC wameendeleza staili yao ya ushindi mwembamba katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo pia kuichapa Mtibwa Sugar 1-0 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.


Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, beki Mghana, Lamine Moro aliyeunganisha kwa mguu wa kulia kona ya chini chini ya kiungo Muangola, Carlos Carlinhos dakika ya 61.


Na kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 10, sawa na mabingwa watetezi, Simba SC ambao wanaendelea kukaa nafasi ya pili kwa faida ya mabao mengi waliovuna baada ya mechi nne za awali.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad