Yanga Yakanusha Kuachana na Suala la Morrison
0
September 04, 2020
Uongozi wa Klabu ya soka ya Yanga umekanusha vikali taarifa zinazoenea kwamba wameliondoa jina la winga Benard Morrion kwenye orodha ya wachezaji wao katika usajili uliokamilika hivi karibuni.
Akizungumza na East Africa Radio ,Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Wakili Saimon Patrick amesema timu yao ilipeleka jina la Bernard Morrison kwenye listi ya wachezaji wao wa 2020/21 lakini wameshangaa kuona Shirikisho la TFF limeondoa jina hilo na kumuacha kwenye listi ya wachezaji wa Simba.
Wakili huyo amesema wao kama Yanga walipeleka jina la Morrison ila wenye mamlaka ambao ni TFF ambao wao wameidhinisha acheze Simba lakini wao wamelipeleka mbele kusaka haki na kesi imeshafika Shirikisho la soka nchini Fifa kwa hiyo wana Yanga wasubiri haki yao.
Katika hatua nyingine wakili Simon ameongeza kuwa wamedhamiria kutwaa ubingwa msimu huu ndio maana wameiweka Timu yao kambini huko Kimbiji kwa msimu wote ili kutimiza matakwa ya Kocha wao Zlatko Krmpotic ambaye alihitaji sehemu tulivu kwa ajili ya kusuka kikosi chake cha ushindi.
"Tumezingatia umuhimu wa msimu ujao kwa malengo yetu ambayo tumejiwekea. Tumeweka kambi huko kwa kuwa Kuna kila kitu ambacho timu inahitaji kama gym, viwanja, sehemu ya kuogelea ndiyo maana tukachagua pale.
"Tumeamua tuhamie pale moja kwa moja tumeona na kwa mfupi na ni sehemu ambayo wachezaji wanaweza kutulia kiakili na wakafanya mazoeI Bila muingiliano wa watu wengine," alisema patrick na kuongeza:
"Pia tutaendelea kufanya mazoezi chuo cha sheria Mawasiliano kwakuwa bado tuna mkataba na lile eneo lakini itategemea na mawazo ya mwalimu."
Vilevile Simon amesisiza kuwa watahakikisha wanakamilisha ujenzi wa Uwanja wao wa mazoezi ili kupunguza gharama za kukodi ambazo fedha hizo zitatumika kwa ajili ya shughuli nyinginezo za Klabu.
Tags