Yanga Yasifia Mziki Wao, Mtibwa Sugar Wajipange



TIMU ya Yanga imeeleza kuwa kazi sasa imeisha baada ya kikosi chao kuonekana kuwa kimeimarika kila idara muhimu.


 

Yanga ilifanya usajili wa wachezaji wengi msimu huu na ilionekana kuwa itawachukua muda kuzoeana lakini uongozi wa timu hiyo kupitia kwa Makamu Mwenyekiti, Frederick Mwakalebela umesema kuwa sasa timu hiyo imeiva.



Yanga ambayo ipo nafasi ya tano ya msimamo wa ligi ikiwa na pointi saba imeshinda michezo miwili na kutoa sare mmoja, inatarajia kushuka dimbani Jumapili kumenyana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa nne wa Ligi Kuu Bara iliyoanza kutimua vumbi Septemba 6.

Akizungumza na Championi Ijumaa,Mwakalebela, amesema kuwa, Kocha Mserbia, Zlatko Krmpotic ameonekana kufurahishwa na kikosi chake ambacho kinampa matumaini ya kufanya vizuri katika kila mchezo ulio mbele yao.


“Kocha amefurahishwa na kikosi kutokana na vijana kuonekana kuimarika siku hadi siku.


“Sasa timu inaonekana kuwa imara baada ya kikosi kuzoeana hasa katika safu ya ushambuliaji, ni matumani yetu tutafanya vizuri zaidi katika mechi yetu dhidi ya Mtibwa Sugar na mechi nyingine zinazofuata.


“Tunahitaji kujipanga kama unavyojua msimu huu tumejipanga tangu awali na tumekuwa vizuri, kufikisha pointi saba si kazi ndogo kama unavyoona wenye pointi tisa na saba ni timu chache hivyo unaona ni jinsi gani tulivyopambana,” alisema Mwakalebela.


Stori: Khadija Mngwai, Dar es Salaam



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad