Zari Ndo’ Basi Tena Bongo!



MWANAMAMA mjasiriamali, raia wa Uganda ambaye ni mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’, ni kama amejipalia makaa ya moto kwa Wabongo, baada ya kumuanika mwanaume wake mpya.


 


Yote hayo yameibuka katikati ya wiki hii, ambapo Zari alikuwa akisherehekea kutimiza umri wa miaka 40.Katika bethidei yake hiyo ambayo ilikuwa Septemba 23, mwaka huu (Jumatano iliyopita), ndipo zikavuja chati za kimapenzi kati ya Zari na mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Fred Nuamah ambaye ni mwigizaji na dairekta mkubwa wa sinema wa nchini Ghana.


 


Ishu hiyo inatajwa kumfuta kabisa Zari kwenye midomo ya baadhi ya Wabongo, kwani sasa amezima zile tetesi kwamba huwenda ipo siku angerejea kwa Diamond au Mondi.




Jamaa huyo ndiye aliyeanza kumuandikia Zari waraka mrefu wenye maneno ya mahaba tele, ambapo Zari naye alishindwa kujizuia na kujikuta namna walivyoanza kuwasiliana kupitia simu ya rafiki yake aliyemtaja kwa jina moja la Eddie.


 


“Maisha yako yanaanza leo, lakini maisha yangu mimi na wewe yalianza siku akiupokea kwa bashasha za kimahaba, huku akimshukuru mwanaume wake huyo mpya kwa kumjali katika siku yake hiyo maalum ya kuzaliwa.


 


Katika waraka huo, aliommwagia Zari kupitia ukurasa wake wa Instagram, jamaa huyo, alianza kwa kuusifia uzuri wa kipekee wa Zari ambaye ni mama wa watoto watano, huku akimweleza kwamba, yeye ndiye mwanamke wa ndoto yake.Jamaa huyo alikwenda mbali zaidi na kuvuta hisia za nilipozungumza na wewe. Nina furaha sana kipenzi cha roho!” Ilisomeka sehemu ya waraka huo na kuendelea;“Mama yao…acha nitumie waraka huu kulifanya penzi letu kuwa jipya…”




Baada ya kuguswa na maneno hayo, Zari au Mama Tiffah alishindwa kujizuia na yeye kujibu mapigo;“Asante baby, nashukuru kuwa na wewe katika maisha yangu, asante kwa kunipenda vile ninavyostahili kupendwa, nakukubali sana…”Majibizano hayo ya kimahaba, ndiyo yaliyowaibua baadhi ya Wabongo kwenye posti hizo ambazo zilisambaa katika kurasa za habari za udaku za Instagram kama moto wa kifuu.


 


Baadhi ya Wabongo hao, walitamka waziwazi kumfuta Zari kwenye mipango yao kwamba, huwenda kuna siku atarejea kwa Mondi.Wengine walikwenda mbali zaidi na kumpongeza Mondi kwa kutokumtakia heri kwenye siku yake hiyo ya kuzaliwa kwa sababu kitendo cha kuibuka kwa mwanaume huyo, kingemdhalilisha na kuonekana anajipendekeza kwa mtu mwenye mtuwe.“


 


Afadhali Simba (Mondi) hajashoboka kumtakia happy birthday, maana huu ungekuwa ni udhalilishaji wa kaka yetu.“Yaani hapa ndo’ Zari amemalizana rasmi na watu wa Madale (familia ya Mondi) na Wabongo kwa sababu hawataki hata kumsikia.


 


“Kwa hiyo Zari anaona anatufokea? Ajue tu hajatufokea chochote, zaidi sana hata sisi (Wabongo) hatutaki kumsikia tena,” ilisomeka sehemu ya maoni lukuki juu ya Zari kumuanika mpenzi wake huyo mpya.Zari na Mondi walitengana mapema mwaka juzi, ambapo hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa huwenda wakarudiana, lakini kutokana na mwanamama huyo kumuweka wazi mtu wake mpya, ni dhahiri kwamba, mapenzi ya wawili hao hayawezi kufufuka, badala yake watabaki kuwa wazazi wenza kwa ajili ya kuwalea watoto wao; Tiffah Dangote na Prince Nillan.Mondi anatarajiwa kufunga ndoa Oktoba 2, mwaka huu, ambayo pia ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad