Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni na Kawe, Aron Kagurumjuli amemtangaza mgombea ubunge wa CCM jimbo la Kinondoni Abass Tarimba ameshinda baada ya kupata kura 112,014.
Tarimba amewashinda wenzake 17 Kati ya hao Suzanna Lyimo wa Chadema amepata Kura 11260 na Said Kubenea wa ACT Wazalendo amepata Kura 5,948.