POLISI Mwanza wanachunguza chanzo cha kifo cha Deogratias Meded (42) Mkazi wa Sengerema aliyefariki dunia muda mfupi baada ya kudaiwa kula makande na chai akiwa kwenye kampeni za mgombea ubunge jimbo la Sengerema kwa tiketi ya CCM, Hamis Tabasamu ambapo Marehemu alikuwa Meneja wa Kampeni wake.
Kamanda wa Polisi Mwanza, Muliro Jumanne, amesema: “Alifariki dunia ghafla akiwa kwenye msafara wa kampeni. Baada ya kula makande na chai alianza kulalamika tumbo linamsumbua. Hali yake ilianza kubadilika ghafla na akafariki dunia kabla ya kuanza kupewa matibabu.”