Afungwa gerezani kwa kumshambulia mwanamke mjamzito kisa ni Mwaisalam



Mwanaume wa Australia aliyempiga ngumi na kumkanyaga mwanamke mjamzito kwa kile kinachoshukiwa kuwa chuki dhidi ya dini yake ya Kiislamu, amefungwa gerezani kwa miaka mitatu

Stipe Lozina, 44, alimshambulia Rana Elasmar, 32, huko Sydney Novemba mwaka jana.

Bi. Elasmar, wakati huo akiwa na ujauzito wa wiki 38, alikuwa na rafiki zake kwenye mgahawa mmoja pale Lozina alipoingia, akasongea kwenye meza yao na kuanza kumuomba pesa.

Baada ya kukataa, moja kwa moja alianza kumrushia maneno yanayoashiria ubaguzi wa kidini, hayo yalisemekana wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Mwendesha mashtaka alisema mshtakiwa alisema kwa sauti ya juu "nyinyi waislamu muliharibia maisha mama yangu" kabla ya kumuangusha Elasmar chini na kuanza kumpiga ngumi mama huyo mjamzito.

Inasemekana kwamba ngumi hizo alizompiga sio chini ya 15 na kumkanyaga nyuma ya kichwa chake kabla ya wateja wengine kufanikiwa kumuondoa juu ya mama huyo.

Akitoa hukumu yake Christopher Craigie awali alielezea kwamba hilo lilikuwa tukio na "kiovu, lisilokubalika na la kusikitisha" na kuongeza kwamba mwanaume huyo bila shaka akili yake haiko sa

"Shambulio hilo lilikuwa na uwezo wa kusababisha maafa makubwa kwa mwathirika na mtoto ambaye hajazaliwa," hakimu alisema.

Bi. Elasmar aliiambia mahakama mwezi Septemba kuwa alihisi amelengwa kwasababu ya dini yake, na kuhofia maisha yake na ya mtoto wake

"Ikiwa hakungekuwa na wa kuingilia kati, ningeliuliuawa," amesema.

"Nilifanya uamuzi wa busara wa kuelekeza tumbo langu kando na sehemu aliyokuwa ananipiga ngumi. Nilitaka kumlinda mwanagu."

Mwanamke huyo alipata majeraha madogo na kujifungua mtoto mvulana wiki tatu baada ya shambulio hilo.

Aidha mahakama ilielezwa vile ambavyo amekuwa na mfadhaiko ikiwemo hofu ya kuwa kwa umma na kuelezea shambulio hilo kwa watoto wake wanne.

"Mashambulizi dhidi ya watu wa dini ya Kiislamu ni lazima yafike mwisho. Ghasia dhidi ya wawanawake lazima zifike kikomo," alisema mwezi uliopita.

Kwa upande mwinginge Lozina ambaye ni mshtakiwa, alikataa kutafuta usaidizi wa kisheria na kujiwakilisha mwenyewe mahakamani.

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake, mara nyingi tu alikuwa anazungumza kwa kubabaika na hata kwa namna isioleweka, vyombo vya habari vya Australia vimesema

Jaji aligundua kwamba alipatikana na ugonjwa wa kuchanganyikiwa kiakili na amekuwa akikabiliana na tatizo la kiakili kwa muda mrefu

Mshtakiwa ataruhusiwa kuachiliwa kwa masharti mwaka 2022 wa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad