KIGOGO wa soka kutoka Morocco, Wydad Casablanca, amekubali kapigika nje-ndani kwenye mtanange wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya bingwa wa kihistoria wa michuano hiyo National Al Ahly ya Misri.
Akiwa nyumbani Wydad alitunguliwa 2-0, juma lililopita na usiku wa jana Ahly akaonyesha umwamba akiwa kwenye uwanja wa nyumbani baada ya kushinda magoli 3-1.
Al Ahly wametinga fainali kwa jumla ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Wydad na sasa anamsubiri mshindi baina ya Zamalek ambaye anaoongoza mechi ya mkondo wa kwanza kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Raja. Mtanange huo utachezwa Novemba Mosi, wakati fainali itachezwa Novemba 6 mwaka huu.
Haya ni mafanikio ya kocha mpya kutoka Afrika ya Kusini, Pitso Mosimane, ambaye amejiunga na Klabu hiyo hivi karibuni akitokea Mamelodi Sundowns.