Aliyekuwa waziri wa Malawi afungwa jela miaka mitano



Mahakama ya juu huko Lilongwe, nchini Malawi imemuhukumu Uladi Mussa, aliyekuwa waziri mwenye ushawishi mkubwa nchini humo kifungo cha miaka mitano gerezani kwa kutumia vibaya madaraka yake.


Mussa alikamatwa kwa kosa la kuwasaidia raia wa kigeni kupata uraia na pasipoti za Malawi kwa njia za ulaghai alipokuwa waziri wa mambo ya ndani chini ya utawala wa aliyekuwa rais Joyce Banda.


Watatu waliokuwa maafisa wa uhamiaji ambao pia walihukumiwa na Mussa, nao wamehukumiwa kifungo cha kati ya miaka mitatu na sita.


Mussa alikuwa mbunge ambaye amehudumu katika nyadhifa mbalimbali za mawaziri chini ya utawala wa marais wanne tofauti.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad