Raia hawa ambao ni maafisa wa Afya waliotumwa Kenya na Cuba kwa makubaliano ya ubadilishanani wa wahudumu wa afya katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.
Madaktari Landy Rodriguez na Herera Correa walivamiwa na wanamugambo hao wa Alshabaab wakitoa huduma za Afya mjini Mandera Kenya uliopo Kazkazini Mashariki na umepakana na nchi ya Somalia. Alshabaab kwa mda wa mwaka mmoja wamewaweka kizuizini mateka hoa huku wakiwaachilia huru hivi leo baada ya kuafikiana mazungumzo baina ya serekali husika kwa mjibu wa ripoti kutoka kwa gazeti la Daily Mail la Ungereza.