Staa wa filamu za mapigano kutoka kiwanda cha filamu cha Hollywood, mkongwe Arnold Schwarzenegger anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo, miaka miwili baada ya upasuaji wa awali.
Mtaalam huyo wa filamu za #Terminator na #EscapePlan ambae pia aliwahi kuonesha mahaba yake katika medani ya siasa baada ya kuwa Gavana wa jimbo la Carlifonia nchini Marekani, alitumia ukurasa wake wa Instagram siku ya ijumaa kuwapa taarifa mashabiki juu ya hali yake, kwenye post aliandika..
“Naishukuru timu (ya wauguzi) ya hapa hospitali ya Cleveland, nina valvu mpya ya aorta kuendana na mrija wangu mpya wa pulmonary, niliowekewa kutoka katika upasuaji wangu uliopita, kwa sasa naendelea vizuri na nimeanza ‘kuzurura’ katika mitaa ya Cleveland nikifurahia majengo na sanamu zenu za kuvutia, shukrani kwa kila daktari na muuguzi kutoka kwenye timu yangu". Aliandika schwarzenegger
Kauli ya ‘Ng’ombe hazeeki maini’ ndio kauli anayotembea nayo mtaalam #Schwarzenegger kwa sasa, kwani licha ya maoni mengi kutoka kwa mashabiki wake wakimtaka apumzike kuigiza filamu, bado staa huyo mwenye umri wa miaka 73 na miezi mitatu anatarajiwa kuonekana tena kwenye screen mbalimbali za sinema duniani, ifikapo Novemba 20 mwaka huu, kwenye filamu mpya ya ‘Iron Mask’ ambapo humo ndani yupo na ‘fundi’ mwingine, Mzee Jackie Chan.