Kwa mujibu wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International limesema, wafanyakazi wa ndani nchini Qatar wanapitia unyanyasaji, kupigwa, kudhalilishwa na mazingira magumu ya kazi.
Taarifa inasema 85% ya Wanawake wanafanya kazi zaidi ya saa 14 kwa siku, hawapewi siku za mapumziko na nyaraka zao za kusafiri zilichukuliwa na waajiri wao walipowasili nchini humo.
Wanawake hao hucheleweshewa mishahara au kutolipwa kabisa, hunyimwa chakula, hulazwa chini, hutemewa mate, hupigwa na kunyanyaswa kingono.
Qatar ni makazi ya wahamiaji milioni 2, wengi wao wakiwa masikini kutoka Bangladesh, Nepal na India, takriban Wanawake 173,000 ni wafanyakazi za nyumbani.