Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama PORI Tanzania Wamuokoa Mtoto Aliepotea Ndani ya Mapori ya Akiba Grumeti



Askari wa Mapori ya akiba Ikorongo/Grumeti wakishirikiana na watumishi wa kampuni ya Grumeti Reserve Ltd pamoja na baadhi ya wanakijiji kutoka vijiji vya Mgeta Maliwanda,Singisi, Sarakwa na Isenye vilichopo wilaya ya Bunda, Mkoani  Mara wamefanikiwa kumpata mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 aitwaye Wakuru Mapinduzi ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Msingi Manyangare wilayani Bunda aliepotea ndani ya mapori hayo ya Akiba.


Meneja wa Mapori hayo ya akiba Bw.Namsifu Johannes Marwa  amesema alipata taarifa za kupotea mtoto huyo kutoka kwa wananchi mnamo tarehe 10/10/2020 na kuagiza askari wa mapori hayo kumsaka mtoto huyo  ili kuokoa maisha yake na kwa juhudi za pamoja mtoto alifanikiwa kupatikana.


Aidha amesema Baada ya kuhojiwa na Askari  wa TAWA alisema kuwa  anatokea kijiji Cha Mgeta na kwamba alipoteza daftari hivyo aliogopa kurudi nyumbani  akaamua kufuata njia ya kwenda kwa jirani yao ndipo akajikuta porini na usiku ukawa umeingia na kufahamu alipotokea na hivyo kumlazima kupotea na kulala siku mbili porini humo.


Hata hivyo Mtoto Wakuru Mapinduzi  alikutanishwa na mzazi wake pamoja na M/kiti wa Kijiji Cha Mgeta na kukabidhiwa katika kituo Cha polisi Isenye kwaajili ya taratibu za kijamii na usalama wa wananchi.


TAWA kupitia uongozi wa Mapori ya akiba ya Ikorongo/Grumeti imekuwa na mahusiano mema na vijiji vyote vinavyozunguka mapori hayo na kila wakati imetoa msaada kwa vijiji vyote vinavyozunguka mapori hayo Mara ilipohitajika kufanya hivyo

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad