Baada ya Yanga Kupata Ushindi Jana Wanne Waingia Kwenye Vita ya Kuwania Tuzo



BAADA ya ushindi wa bao 1-0 walilopata Yanga jana Uwanja wa Uhuru na kusepa na pointi tatu nyota wanne waingia kwenye vita ya kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mechi.

Bao pekee la ushindi kwa Yanga inayonolewa na Cedric Kaze raia wa Burundi lilipachikwa kimiani na Tonombe Mukoko dakika ya 70 kwa pasi ya Farid Mussa.


Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 16 kibindoni baada ya kucheza mechi sita na inawashusha Simba nafasi ya pili kwa kuwa walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela.


Wachezaji wanaowania tuzo ni pamoja na Farid Mussa, Tunombe Mukoko, Bakari Mwamnyeto na Yassin Mustapha. 


Ikiwa imecheza mechi sita Yanga imeshinda mechi tano na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons.


Imefunga jumla ya mabao nane na kufungwa bao moja kwenye mechi sita za ligi ambazo imecheza kwa msimu wa 2020/21.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad