Bad News: Katibu Mwenezi Chadema Auawa Singida



Katibu Mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kata ya Mhintiri, Jimbo la Singida Magharibi, Nicholas Andrea Gui, amekutwa ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana jana, Jumanne, Oktoba 7, 2020, majira ya saa moja jioni.


 


Taarifa hiyo imetolewa na Hemedi Kulungu mgombea ubunge Singida Magharibi (Chadema) ambaye amesema: “Katibu Mwenezi wa Chadema Kata ya Mhintiri, Jimbo la Singida Magharibi ameuawa kwa kukatwakatwa na mapanga kwenye mashamba yake. Amepatikana akiwa amefariki. Nimepata taarifa wakati huu nikitoka kwenye mkutano wa kampeni Kijiji cha Mayaha, Kata ya Minyughe. Nimewasiliana na OCD Wilaya ya Ikungi,” amesema Kulungu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad