Baraza za Ulamaa BAKWATA Taifa chini ya Mwenyekiti, Mufti Sheikh Abubakar Zubeir Mbwana ambaye pia ni Sheikh Mkuu wa Tanzania limetoa maelekezo kutokana na yanayojitokeza katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu
Limewasihi Viongozi wa Dini kubaki kuwa wasuluhishi na wapatanishi wa jamii inayowahusisha wafuasi wa vyama na wasio na vyama
Pia limewataka Viongozi wote wa Baraza kutofanya Kampeni, hasa katika nyumba za ibada, na wanaoenda kinyume na mafundisho ya Uislamu na maadili ya BAKWATA watachukuliwa hatua za kinidhamu
Aidha, limewataka Waislamu kuiombea nchi ili Uchaguzi Mkuu upite salama na kwa amani