Benki ya Dunia yaidhinisha mabilioni ya dola kwa ajili ya chanjo ya COVID-19 kwa nchi masikini



Benki ya Dunia jana imeidhinisha kiasi dola bilioni 12 kwa mataifa yanayendelea ili kugharamia ununuzi na usambazaji wa chanjo, vipimo na matibabu ya ugonjwa wa COVID-19.

Taarifa iliyotolewa na benki hiyo imesema fedha hizo ni sehemu ya mpango jumla wa msaada wa dola bilioni 160 utakaotolewa hadi katikati ya mwaka 2021 kuzisadia nchi masikini kukabiliana na janga la virusi vya corona.


Msaada huo wa kifedha utakaowanufaisha karibu watu bilioni 1, utafadhili utafiti kwa kampuni za utengenezaji dawa pamoja na kuratibu matayarisho ya kupokea na kusambaza chanjo za COVID-19 kwenye mataifa yanayoendelea


.Ingawa bado hakuna chanjo ya COVID-19, Benki ya Dunia imesema ni muhimu kwa mataifa hayo kujiweka tayari kwa sabbau usambazaji wa chanjo ni mchakato wenye vikwazoi visivyotabirika

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad