Bomu hatari la 'mtetemeko' la vita ya pili ya dunia lalipuka kabla ya kuteguliwa Poland



Bomu kubwa ambalo halikulipuka katika vita ya pili ya dunia lililobainika nchini Poland limelipuka wakati wa shughuli ya kulitegua, msemaji wa jeshi la wanamaji nchini humo ameeleza.

Uwezekano wa bomu hilo lililokuwa chini ya bahari kulipuka ulikuwa ukitarajiwa na wapiga mbizi wote waliohusika kwenye tukio hilo hawakujeruhiwa.


Karibu wakazi 750 waliondolewa karibu na mji wa bandari wa Swinoujscie.


Bomu hilo liitwalo Tallboy au ''tetemeko la ardhi'' lilidondoshwa wakati wa vita ya pili ya dunia na kuizamisha meli ya Ujerumani Lützow.


Swinoujscie ilikuwa sehemu ya Ujerumani na kuiita Swinemünde wakati wa ulipuaji.


Wanajeshi wa Poland kutegua bomu kubwa la vita vya pili vya dunia


Mtikisiko wakati wa kulitegua bomu hilo ulisikika katika sehemu za mji na video zinaonesha mlipuko mkubwa na maji mengi yakiruka angani.


Bomu hilo lilikuwa na urefu wa mita 6 na uzito wa tani 5.4, karibu nusu ya bomu hilo liliundwa na vilipuzi.


Lilikuwa limetua kwenye kina cha mita 12 na sehemu ya pua ya bomu hilo ilikua ikichungulia nje.


Jeshi la wanamaji walitumia chombo kilichokuwa kikidhibitiwa kutoka mbali kwa ajili ya kujaribu ''kuchoma'' bomu hilo - mbinu ambayo kama ikifanikiwa huchoma mifumo ya chaji za vilipuzi bila kusababisha mlipuko, mwanahabari wa BBC Adam Easton anaripoti kutoka Warsaw.


''Mbinu hiyo ya kuchoma iligeuka mlipuko. Chombo hicho kimeelezwa kuwa kimepozwa, hakitasababisha tishio lolote tena kwa njia za meli za Szczecin-Swinoujscie,'' alisema Luteni kamanda Grzegorz Lewandowski, msemaji wa jeshi la maji wa gadi ya nane ya ulinzi wa pwani Flotilla.


''Wapiga mbizi wote walitoka katika eneo la hatari wakiwa salama.''



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad