MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Arusha Mjini amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda kata 24 kati ya 25 za udiwani katika jimbo hilo.
Aidha, upande wa ubunge, tume bado inaendelea na majumuisho ya kura, na wamefikia kata ya 14 hivyo si muda mrefu watatoa matokeo ya Ubunge.
Jimbo hilo lina mchuano mkali kati ya wagombea wawili ambao ni Mrisho Mashaka Gambo wa CCM na Godbless Lema wa Chama cha Demokrasiana Maendeleo (Chadema).