‘
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilwa Kusini kwa tiketi ya ACT WAZALENDO na Mbunge aliyemaliza muda wake wa Jimbo hilo Selemani Bungara Maarufu kwa jina la Bwege (aliyeshika Ipad kushoto) akifuatilia kwa makini hotuba ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa wakati alipomuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Wabunge na Madiwani wa CCM kwenye uwanja wa Ukote, Kilwa Kivinje mkoani Lindi, Oktoba 22, 2020.
MGOMBEA UBUNGE wa jimbo la Kilwa Kusini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Bw. Selemani Bungara maarufu kwa jina la Bwege ameukubali muziki wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kufatilia kwa makini hotuba zake.
Bw. Bungara ambaye katika kipindi kilichopita alikuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Wananchi (CUF), amehudhuria mkutano wa kumuombea kura mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM wa jimbo hilo uliofanyika leo (Alhamisi, Oktoba 22, 2020) kwenye uwanja wa Ukote, Kilwa Kivinje, wilayani Kilwa, mkoani Lindi.
Mbunge huyo aliyemaliza muda wake katika jimbo hilo, alionekana akirekodi kwa kutumia simu yake huku akifuatilia kwa makinik hotuba ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa wakati alipomuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Wabunge na Madiwani wa CCM
Akizungumza na wakazi hao, Mheshimiwa Majaliwa aliwataka wakazi wa Kilwa wamchague mbunge ambaye atakuwa tayari kupitisha bajeti na kuwaletea maendeleo.
“Tanzania inahitaji watu makini na pale Bungeni siyo mahali pa vichekesho. Bunge linahitaji watu wa kuwasemea wananchi na siyo kuleta burudani wakati wengine wako kazini,” amesema.