Carlinhos Amfunika Jumlajumla Morrison



HUKU kukiwa na fukuto la mkataba wake likiwa limeanza upya ndani ya klabu yake ya zamani ya Yanga wakidai kuwa mkataba wake ni batili ndani ya Simba, rekodi zinaonyesha kuwa kiungo Bernard Morrison amepotezwa jumlajumla na Carlos Carlinhos wa Yanga kwa upande wa pasi za mwisho.


Ndani ya dakika 137, Carlinhos amempoteza Morrison kwa upande wa pasi za mwisho ambapo yeye ni kinara ndani ya Yanga akiwa nazo mbili huku Morrison akiwa na pasi moja ya bao ndani ya dakika 181.



 

Ujanja wa Morrison ni Uwanja wa Mkapa ambapo pasi yake ya kwanza ndani ya ligi akiwa Simba alimpa Chris Mugalu wakati Simba ikishinda mabao 3-0 mbele ya Gwambina FC huku Carlinhos akipeta kwa Mkapa kwa kumpa pasi Lamine Moro kwenye ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mbeya City na ya pili alitoa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakati Yanga ikishinda bao 1-0.


Carlinhos amepiga jumla ya kona 11 ambapo 5 mbele ya Mbeya City, 2 mbele ya Kagera Sugar na 4 dhidi ya Mtibwa Sugar. Katika hizo mbili zilisababisha mabao.


Morrison alipiga kona 3 mbele ya Ihefu na moja mbele ya Gwambina FC akiwa amepiga jumla ya kona nne hakuna hata moja iliyosababisha bao.


Mechi za Carlinhos zilikuwa:- Mbeya City alicheza kwa dk 30 Uwanja wa Mkapa, Kagera Sugar dk 35 Uwanja wa Kaitaba, dk 72 mbele ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri.


Morrison alitumia dk 67 mbele ya Ihefu Uwanja wa Sokoine, dk 66 mbele ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, dk 25 mbele ya Biashara na dk 23 mbele ya Gwambina zote Uwanja wa Mkapa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad