CHADEMA yatangaza kumuunga mkono Maalim Seif

 


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema baada ya Kamati kuu kukaa kikao,kimeona ni sahihi kwa chama hicho kumuunga mkono Mgombea Urais kupitia Act Wazalendo kwa upande wa Zanzibar Maalim Seif Sharif. 


Akizungumza hii leo Oktoba 4,2020 katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika  makao makuu ya chama hicho Kinondoni jijini Dar es salaam  Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe,amesema vyama kushirikiana ni suala ambalo linajenga umoja na mshikamano katika nchi.


''Sisi kama Kamati kuu tumeridhika na kauli mbalimbali zilitolewa na viongozi wa vyama vyetu  hususani CHADEMA na ACT-Wazalendo na baada ya kushauriana na mgombea wetu wa zanzibar Mhe.Said Issa Mohammed  tumeona ni sahihi kwa Chama chetu kumuunga mkono  Seif Sharif Hamad''amesema  Freeman Mbowe 


''Mgombea wetu katika kinyang'anyiro cha Urais Zanzibar ambaye ndiye aliyekuwa ameteuliwa kugombea ameridhia kwamba yeye atajitoa na atamwachia Maalim Seif Sharif Hamad awe mgombea ambaye sisi tutamuunga mkono katika uchaguzi wa Zanzibar''ameongeza


Aidha Mbowe amesema kuwa kama chama hicho kitajiridhisha kuwa kimeshindwa kihalali kitakubali matokeo.


 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad