Chama tawala Sudan chashtakiwa kwa kunyima wanawake nafasi za uongozi



Wanaharakati wanataka Rais Salva Kiir (katikati) kubalisha magavana wawili aliowachagua na wanawakeImage caption: Wanaharakati wanataka Rais Salva Kiir (katikati) kubalisha magavana wawili aliowachagua na wanawake

Kundi la wanaharakati nchini Sudan Kusini limeshitaki chama tawala cha Sudan People’s Liberation Movement (SPLM), katika mahakama ya juu kabisa kwa kile wanachosema ni ukiukaji wa haki za wanawake kulingana na katiba.


Walishtumu chama hicho kwa kutoheshimu katiba na ukiukaji wa Makubaliano ya Amani ya 2018 ambayo yanahakikisha wanawake asilimia 35 ya nafasi za uongozi katika ngazi zote za serikali.


Ombi hilo lilipokelewa na naibu jaji mkuu, John Gatwich Lul, aliyeahidi kuliwasilisha kwa Jaji Mkuu, Chan Reec Madut, ili kuzingatiwa.


Juni, Rais Salva Kiir aliteuwa magavana 9 katika majimbo 10 nchini humo. Mmoja pekee ndio mwanamke, Sarah Cleto Rial, aliyechaguliwa na chama cha naibu rais wa kwanza Riek Machar.


Chama cha rais hakikumteua mwanamke yeyote katika nafasi zake sita za ugavana.


“Tunasihi mahakama ya juu zaidi kutoa agizo kwa chama cha SPLM na kuwalazimisha kuondoa magavana wawili wanaume na nafasi hizo zipewe wanawake,” Wani Michael, mlalamishi amezungumza na BBC katika mji mkuu wa Juba, Alhamisi.


Bwana Wani amesema ikiwa mahakama itashindwa kuchukua hatua ya kuzingatia ombi lao, kuna uwezekano wa kulipeleka katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki mjini Arusha nchini Tanzania.


Sudan Kusini ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini bado haijathibitishwa kuwa mwanachama kamili.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad