Chanzo cha ajali ya ndege ya Ukraine chabainika



 Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Oleg Uruskiy, alisema kuwa chanzo cha ajali ya ndege ya kijeshi iliyoanguka katika mji wa Kharkiv mnamo Septemba 25, kilikuwa ni hitilafu za kiufundi na ukiukaji wa taratibu za kikazi.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, Uruskiy alibaini kuwa wawakilishi 3 wa tume ndogo ya uchunguzi wa anga, ndege na ufundi walimpa ripoti ya ajali hiyo.


Akibainisha ajali hiyo kusababisha na hitilafu ya injini ya kushoto na kihisio cha presha, Uruskiy pia alifahamisha kwamba kulikuwa na ukiukaji wa taratibu za kurusha ndege zilizovuruga mpangilio.


 Uruskiy pia alisema kuwa tume ya Uchunguzi kutoka serikalini bado inaendelea na shughuli yake.


Ajali ya ndege hiyo aina ya AN-26 ilitokea mnamo tarehe 25 Septemba mjini Kharkiv nchini Ukraine, na kusababisha vifo vya watu 26 na majeruhi mmoja.


Ndege hiyo ilikuwa ikirushwa kwa ajili ya mafunzo ikiwa imebeba wafanyakazi pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kikosi cha Anga cha Kharkov.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad