Ni muendelezo wa matukio ya msanii pendwa wa HipHop hapa nchini Tanzania, Chidi Benz ambaye amemtambia Country Wizzy mbele ya 'Bodyguards' wake wakati walipokutana kwenye show ya Friday Night Live ya East Africa TV.
Sasa haya hapa ni baadhi ya maneno ambayo ameyatamka Chidi Benz baada ya kumuona Country Boy akiwa na 'Bodyguards' wake.
"Itabidi uwatengeneze hawa Bodyguard kwa mtindo ambao watu wakiwaona wawashangae kwa jinsi ambavyo watakavyovaa, kwanza wawe tofauti kuanzia saa, raba hadi 'timberland' ili wakionekana watu wajue kabisa wale ni watu wake Country Boy sio wa Harmonize, au hata promota wa show akikuona atamani kufanya biashara na wewe" amesema Chidi Benz