Viongozi wa China watajadili muelekeo wa uchumi wa taifa lao katika kipindi cha mwaka 2021-2025, katika mkutano wao muhimu ambao unatarajiwa kuanza Jumatatu ijayo.
Miongoni mwa mambo mengine viongozi hao wanatarajia kuweka uwiano na mabadiliko katika jitihada za kuepuka mkwamo, katika kipindi hiki ambapo kumekuwemo na mtazamo usio sawa wa kidunia na kuongezeka kwa mvutano wa taifa hilo na Marekani.
Rais Xi Jinping na wajumbe wa Kamati Kuu ya chama tawala cha Kikomunisti watakutana Oktoba 26 hadi 29, katika mkutano wa ndani, na kuweka muongozo wa taifa hilo wa 14, ambao utaelekeza kuhusu uchumi na maendeleo ya jamii.