CUF wafungiwa kwa siku 10 kufanya kampeni jimbo la Mtwara mjini


 

Chama cha Wananchi CUF Jimbo la Mtwara Mjini wamefungiwa kufanya kampeni kwa siku kumi kuanzia leo Oktoba 10 mwaka 2020.


Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya maadili wa tume ya uchaguzi Jimbo la Mtwara Mjini ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara Mikindani, Kanali Emanueli Mwaigobeko.


Mwenyekiti huyo amesema kuwa aliipokea barua kutoka Chama cha Mapinduzi wakilalamikia juu ya ukiukwaji wa maadili ya Uchaguzi wa Rais ,Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 unaofanywa na Chama hicho.


Kamati ya maadili ya Uchaguzi Jimbo la Mtwara Mjini baada ya kupokea barua ya malalamiko siku za nyuma imeketi kikao mnamo Otoba 9 mwaka huu ili kujadili malalamiko hayo ambapo Chama cha CUF kilikili kuyafanya makossa huku wakisema kuwa walifanya hivyo kwa kuwa kuna baadhi ya vyama navyo vinafanya matukio kama hayo.


Mara baada ya kuyapitia malalamiko hayo, utetezi na ushahidi, kamati ya maadili Jimbo hilo imeridhishwa kuwa Chama cha wananchi CUF Jimbo la Mtwara Mjini kimekiuka maadili ya Uchaguzi ya Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 kwa kutumia lugha za matusi, kashfa, kejeli, udhalilishaji na lugha inayochochea uvunjifu wa amani.


Aidha kamati hiyo ya maadili imetoa uamuzi dhidi ya Chama cha wananchi CUF Jimbo hilo kwa kusimimishwa kufanya kampeni kwa muda wa siku kumi kuanzia leo tarehe 10 Oktoba 2020 mpaka tarehe


Msimamizi huyo amewataka wagombea na viongozi wa vyama vya Siasa Jimbo la Mtwara Mjini  kufuata maadili na kanuni za Uchaguzi.


''Chama cha CUF Jimbo la Mtwara Mjini  kinapaswa kuomba Umma msamaha kwa makosa hayo ya ukiukwaji wa maadili ya Uchaguzi huo wa Rais,Wabunge na Madiwani kwa mwaka 2020'' amesema Kanali Mwaigobeko

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad