Diamond Hakamatiki, Grammy Wamvulia Kofia



VICHWA vya habari vikubwa kutoka kwa staa wa muziki kutoka Tanzania na Barani Afrika kwa ujumla Diamond Platnumz, baada ya kufanyiwa mahojiano maalumu na waandaaji wa Tuzo kubwa duniani za Muziki GRAMMYs.


Kupitia website yao pamoja na kurasa zao za mitandao ya kijamii, Grammy wamemuelezea Diamond kama mwanamuziki aliyeweza kubadilisha taswira ya muziki wa Afrika Mashariki pamoja na kufikia viwango ambavyo ni ndoto ya kila mwanamuziki kufika.


Grammys Pia wamesifu jitahada za Diamond, kuweza kuongezea radha za Kiingereza na Kiswahili, taarabu, R&B na Caribbean, nyimbo za slow na za kishisia, katika muziki wa “BongoFleva” kitu kilichofanya aweze kuvuka mipaka tofauti na watangulizi wake, ambao wametajwa kuwa ni Dully Sykes, Juma Nature, TID na Q Chief.


Haya ni baadhi ya mambo yaliyomfanya kutusua kimuziki na kufanikiwa kazi na Wasanii wakubwa duniani kama vile Omarion (“African Beauty”), Rick Ross (“Waka”), Ne-Yo (“Marry You”) and most recently, Alicia Keys (“Wasted Energy”).


Tuzo za Grammys ndio Tuzo kubwa zaidi za Muziki Duniani na ndoto ya kila mwanamuziki! Hivyo kitendo cha waandaaji wa Tuzo hizi kumzunguzia na kumpa heshima Diamond, ni ishara nzuri kwa Muziki wa Afrika Mashariki.


Grammy wameendelea kutaja ngoma za Mondi zilizotikisa zaidi ni; Number One, Kamwambie, Kidogo, Sikomi, Inama, Baba Lao, Nana na Jeje.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad