Web

Dully Sykes ametangaza ujio wa lebo yake ya muziki



Nyota wa muziki wa Bongo Fleva, AbdulWahid Sykes Prince Dully Sykes ametangaza ujio wa lebo yake ya muziki itakayoitwa ‘Misifaz Music’ ambayo itakuwa inasaidia wasanii kutoka kimuziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dully ametangaza neema kwa wasanii wa muziki ambao walikuwa na matamanio ya kuongozwa na kusimamiwa kimuziki na mwanamuziki huyo mkongwe aliyejizolea umaarufu nchini kutokana na nyimbo zake.


Dhumuni la kuanzisha lebo hiyo ni kuwasaidia wasanii wachanga ambao hawajatoka kimuziki hivyo anataka kuwasaidia kwa kuwatambulisha kwa watanzania. Ameeleza #Dully kwenye kipindi cha 'The Switch', Wasafi FM.


Ujio wa lebo hii mpya ya muziki nchini, #DullySykes ataungana na wasanii kama AliKiba, Diamond, Harmonize, Vanessa Mdee, Joh Makini na wengine ambao tayari wana Lebo za muziki zinazo wasimamia wasanii.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad