Ethiopia yawakamata watu 500 kabla ya tamasha la jamii ya Oromo, fahamu zaidi



Mamlaka katika jimbo la Oromia lililo na watu wengi zaidi nchini Ethiopia zinasema kuwa zimewakamata watu 500 wanaodaiwa kupanga njama za kufanya vurugu wakati wa tamasha la kutoa shukrani linaloandaliwa kila mwaka maarufu Irreecha, kwa jamii ya Oromo nchini humo.




Kamishna wa polisi katika jimbo la Oromia,Ararsa Merdasa siku ya Alhamisi alisema kando na watu hao pia wamenasa silaha kadhaa za moto ikiwa ni pamoja na bunduki ndogo aina ya pisto na guruneti ya kurusha kwa mkono.


Hatua ya kukamatwa kwao inajiri baada kuongezeka kwa taharuki za kisiasa nchini humo.


Tamasha hilo litaandaliwa Jumamosi na Jumapili katika mji mkuu, Addis Ababa, na maeneo tofauti na jambo la Oromia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad