Msaikolijia kutoka Chama cha Wanasaikolojia Tanzania, Neema Kessy, amesema kukosa kupata muda wa kupumzika kuna changia katika kuzorotesha afya ya akili.
Akizungumza katika kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, Neema, amesema kuwa kupata muda mzuri wa kupumzika kuna changia katika kuboresha afya ya akili.
“Kutokupata muda mzuri wakupumzika limekuwa tatizo kwa watu wengi sana, tunapumzika kidogo kwasababu mbalimbali ambazo tunazipata kwa ajili ya kusaka kipato, tunatakiwa tuhakikishe tunapata muda wa kutosha wa kupumzika huo utatufanya afya yetu ya akili ikae vizuri” amesema Neema Kessy
Aidha Msaikolojia huyo ameitaja michezo kuwa mmoja ya kigezo kinachosaidia kustawisha si tu afya ya mwili bali na akili pia, “Kufanya mazoezi itakusaidia kufanya afya ako ya mwili iwe vizuri lakini na afya ya akili nakukuondelea yale magonjwa yasiyoambukiza ambayo watu wengi walioingia kwenye magonjwa yasiyoambukiza yameathiri afya yao ya akili" amesema Neema Kessy