"Fatilieni uraia, kuna watu siyo wenzetu"-Polepole

 


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, (CCM), Hamphrey Polepole, amewaomba wapiga kura nchini kuwa wahakikishe wanafuatilia uraia wa baadhi ya wagombea katika uchaguzi mkuu ujao kwa madai ya kuwa wana nia ya kuleta vurugu na kuondoka.


Polepole ametoa kauli hiyo hii leo Oktoba 17, 2020, jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wake wa kampeni na waandishi wa habari, ambapo pia ametoa tathmini ya kampeni zilizofanywa na chama hicho mpaka sasa.


"Yule mgombea wa chama cha Mbowe ameshawaambia kabisa watoto wake hawawezi kusoma shule za kata na video yake ipo, na niwaambieni kuna wagombea fuatilieni uraia wao kuna watu hapa siyo wenzetu, wametega tu walete vurugu kisanuke hapa halafu wao shaa!! wanakuwa wanatuangalia kwenye TV, mjomba hii haikubaliki sisi tumezaliwa na tutakufa hapa hapa", amesema Polepole.


Aidha Polepole ametoa tathmini juu ya mgombea Urais wa chama hicho, "Kabla ya kupiga kampeni CCM, ushindi wake haupungui asilimia 75 na kamati ya ushindi ya CCM, ilikuwa imejiwekea malengo yake kura za urais ni asilimia 90, unagundua ndugu Magufuli alianza ukanda mmoja, Samia Uganda mwingine, tukachukua makada waandamizi wa chama wakaenda upande mwingine".

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad