Harmonize Alizwa Mamilioni YouTube



Staa wa Bongo Fleva ambaye pia ni bosi wa lebo kubwa ya muziki nchini Tanzania ya Konde Gang Music Worldwide, Rajab Abdul ‘Harmonize’, amelizwa na kitendo cha upotevu wa mamilioni tangu kuondolewa (terminated) kwa akaunti ya YouTube ya memba wa lebo yake hiyo, Ibrahim Abdallah ‘Ibraah TZ’.


 


Akaunti hiyo iliondolewa siku chache zilizopita huku sababu za msingi zikiwa hazijajulikana hadi sasa huku ikisemekana ni matatizo ya kiufundi.Nyimbo zote za Ibraah hazipo kwenye akaunti hiyo, bali ile aliyomshirikisha Harmonize au Harmo tu ya One Night Stand ambayo iko kwenye chaneli ya Harmo.


 


MAMILIONI YAPOTEA


Lebo hiyo imepata pigo kubwa la kupoteza mamililioni kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika kwa Ibraah kama msanii wa kwanza kusainiwa na Konde Gang.


 


Siku chache tu baada ya kusainiwa kwake, Ibraah aliachia Extended Play (EP), yenye nyimbo tano na zote zikifanya poa kwa kukimbiza na kuingiza kiasi kikubwa cha pesa kwenye mitandao ya kuuza, kupakua, kutazama na kusikiliza muziki (platforms) ikiwemo Mtandao wa YouTube.




Nyimbo zote hizo ambazo zimeonekana kufanya vizuri kwa kupendwa na hata kuiingizia mapato makubwa lebo hiyo, nazo zimeathiriwa kutokana na tatizo la kushushwa kwa akaunti, ishu ambayo imesababisha lebo kupungukiwa mapato yaliyokuwa yakiingizwa na akaunti ya Ibraah ambayo nayo ilikuwa inaingiza malipo ya nyimbo zinazosikilizwa na kutazamwa mno kwenye YouTube.


 


MITANDAO INALIPAJE?


Mitandao ya muziki na kazi za wasanii huwa ina utaratibu wa kuainisha mapato ya kila msanii kutokana na kazi zake ambapo msanii wa Kobongo anayesikilizwa au kutazamwa zaidi anaweza kuingiza hadi Dola 15,000 kwa mwezi ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 30 za kitanzania.


 


Kupitia ishu hiyo, Ibraah atakuwa tayari amepoteza mamilioni ya kulipwa kwenye nyimbo zake zilizo kwenye Mtandao wa YouTube.


 


MENEJA AFUNGUKA


Ili kupata ukweli wa mambo, Gazeti la IJUMAA lilimtafuta mmoja wa mameneja wa lebo hiyo, Almasi Mzambele ambapo aliweka wazi kuwa, wao kama mameneja, hawawezi kuzungumza juu ya suala hilo, bali Harmo mwenyewe.


 


“Kwa upande wetu sisi kama mameneja, hatuwezi kuzungumzia chochote juu ya ishu hiyo.“Hivi karibuni Harmonize mwenyewe atakuja kutoa ufafanuzi juu ya hili na watu wataelewa yote kuhusiana na ishu ya kushushwa kwa akaunti ya Ibraah,” anasema Mzambele.


 


MASHABIKI WAFUNGUKA


Baadhi ya mashabiki wa Konde Gang wamefunguka juu ya ishu ya kushushwa kwa akaunti hiyo na kusema kuwa Harmo ajipange maana ni hasara tu.“Dah! Yaani Harmonize atakuwa amepata hasara kutokana na ishu hiyo maana Ibraah ndiyo kwanza msanii wa kwanza kusainiwa na lebo imewekeza sana kwenye ishu hiyo,’’ alisema Shabiki mmoja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad