Hotuba za Hitler Zapigwa Mnada



HOTUBA nane za kiongozi wa zamani wa Ujerumani, Adolf Hilter, zimepigwa mnada mapema leo kwenye Jiji la Munich, kwa kwa dola za Marekani 40,300 ambazo ni sawa na zaidi ya  milioni 92 za Kitanzania.

 Hiltler ambaye aliziandika kwa mkono hotuba hizo wakati wa Vita ya Pili ya Dunia (WW2), zilikutwa baada ya muungano wa vikosi vya Ulaya vikiiongozwa na Urusi kuvamia handaki alipokuwa amejificha.

 Nakala za hotuba hizo zimeuzwa huku kukiwa na hofu kubwa kuwa huenda zikaamsha hisia zilizolala za Wayahudi kutoka Israel.  Itakumbukwa kuwa kwa amri ya Hilter inakadiriwa Wayahudi milioni sita waliuawa kati ya mwaka 1941-45.

 Makundi mbalimbali ya Wayahudi kwenye mitandao ya kijamii, wamesema  kuuza hotuba hizo ni sawa na kuuza utu wa Myahudi.  Mpaka sasa serikali ya nchi hiyo haijatoa taarifa yoyote juu ya hatua hiyo ya Ujerumani.

 Kiongozi huyo wa aina yake kuwahi kutokea kwenye historia anakumbukwa kwa hotuba zake zilizokuwa na ushawishi mkubwa na jinsi alivyokuwa katili kwa watu waliopinga sera zake.

 Inaaminika hotuba hizo aliziandika  kwenda kwa maafisa wa jeshi miezi minane kabla ya kuanza kwa Vita ya Pili ya Dunia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad