Jaqueline Mengi Aeleza Siri Ya Umiss Kupoteza Umaarufu




WAKATI mashindano ya urembo nchini yakiwa yanaendelea kupoteza mvuto aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2000, Jaqueline Mengi ametaja baadhi ya sababu walimbwende wa Tanzania kushindwa kutoboa katika mashindano hayo kwenye duniani.


 


Akizungumza na paparazi wetu Jaqueline alisema miongoni mwa mambo yaliyoyapoteza mashindano hayo ni kuongezeka kwa vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikisapoti burudani nyingine.


 


“Kipindi cha nyuma vyombo vya habari vilikuwa vichache na vilipoandika kuhusu Miss Tanzania kila mtu alikuwa akifuatilia habari hiyo lakini sasa hivi vyombo ni vingi na vimekuwa vikiandika habari tofauti.


 


“Sasa hawana muda wa kukaa na kufuatilia mashindano ya mamiss wakati kwenye mitandao ya kijamii kuna mambo kibao ya kufuatilia.


 


“Jambo lingine lililoyapoteza mashindano haya ni kukosekana kwa wadhamini wa kuyasimamia na hivyo kukosa mwelekeo na kuvutia kama siku za nyuma.


 


“Kipindi hicho ilikuwa siku ya fainali za miss Tanzania watu walikuwa hawalali walikesha kwenye runinga mpaka wamjue mshindi.


 


“Kabla ya kupatikana msindi ulikuwa ukiibuka ubishani mkubwa kila upande ukisema fulani ndiye atanyakua taji hilo na mwisho wa siku kweli taji lilienda kwa mmoja wapo na wote walibaki kumpa saluti,” alisema Jaqueline.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad