Jeshi la Marekani limeonesha miwani ya ukweli inayovaliwa na mbwa wa kijeshi, iliyoundwa ili kupokea maagizo kwa mbali.
Teknolojia hiyo, iliyotengenezwa na kampuni inayoitwa Command Sight, inasimamiwa na Maabara ya Utafiti wa Jeshi la Marekani.
Mbwa wa kijeshi wanaweza kubaini vilipuzi na vitu vingine hatarishi lakini wanahitaji kupatiwa maagizo.
Miwani imeundwa ili kuwaruhusu wanaowadhibiti kuwapa maelekezo , kwa usalama.
Katika shughuli za kijeshi, wanajeshi kwa kawaida huwaongoza wanyama kwa ishara za mikono au vifaa vya kuwaonesha- ambavyo vinalazimu muongozaji kuwa karibu na mnyama.
Lakini hali inaweza isiwe hivyo kama mawani maalumu ya prototype AR itatumika, jeshi limesema.
Ndani ya mawani, mbwa wanaweza kuona maelekezo ambayo wanaweza kufundishwa kuyafuata, yakiwaongoza sehemu husika.
Muongozaji, wakati huohuo, anaweza kuona anachokiona mbwa kupitia video.
''Mawani ya AR itatumika kuwapa mbwa amri na miongozo'', alisema Dkt Stephen Lee, Mwanasayansi mwandamizi wa maabara ya kijeshi (ARL)
Alieleza kuwa mawani hiyo inafanya kazi kwa mbwa zaidi kuliko binadamu, aliongeza: ''Jamii ya mbwa wa kijeshi inafurahia kuhusu umuhimu wa taknolojia hii.''
Kila mawani humtosha mbwa, ikimuwezesha mbwa kutazama maelekezo kuelekea kwenye eneo lengwa na kufanyia kazi maelekezo kwa picha anayoyaona ndani ya mawani.
Mawani yenyewe sio mpya - mbwa wa kijeshi tayari wamezoea kuzivaa kama kinga katika mazingira mabay
Mwanzilishi wa mradi wa taasisi ya Command Sight amesema mradi huo bado ulikuwa katika "hatua za mwanzo za utafiti", lakini matokeo ya mapema yalikuwa "ya kutia moyo sana".
Utafiti mwingi ulikuwa umefanywa na mbwa wake mwenyewe aliyeitwa Mater.
Justin Bronk, mtafiti mwenza katika taasisi ya ulinzi ya Royal United (Rusi), aliambia BBC kwamba ingawa wazo hilo linaweza kuonekana kama "gharama kubwa", bado linaweza kuwa na faida.
"Uwezo wa kuelekeza mbwa kupitia miwani bila ya mbwa na mwelekezi kuwa una faida dhahiri za kimkakati katika hali mbalimbali,'' aliongeza