Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. John Magufuli, amewakumbusha wananchi namna alivyopitia wakati mgumu katika kufanya maamuzi kwa maslahi ya taifa katika kipindi cha miaka yake mitano ya urais.
Dk. Magufuli ametoa kauli hiyo alipokuwa akiongea kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kinyerezi Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema amejitoa mno kwa ajili ya Watanzania na sasa anaomba wamchague tena amalizie kazi.
Dk. Magufuli amesema watu waliokuwa wakijinufaisha na rasilimali za nchi hawafurahishwi na hatua alizochukua za kulinda rasilimali za nchi tangu aingie madarakani na wamemfanya yeye kuwa adui wao namba moja.
“Watu wengi wanaonea wivu nchi yetu kutoka na kuwa na utajiri wa rasilimali pamoja na miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea nchini kwa kuwa hawakutarajia ingewezekana,” alisema Dk. Magufuli.
Alitaja baadhi ya hatua zilizompatia maadui kuwa ni mabadiliko aliyoyafanya katika sekta ya madini pamoja na kuzuia kusafirishwa nje makinikia, kujenga uzio kwenye machimbo ya Tanzanite, ujenzi wa mradi wa kufua umeme Selous na kutochukua hatua za kufungia wananchi ndani wakati wa Corona