JPM Afichua Aliyokata Jina la Mtoto wa Dada Yake ‘Nikamteua Gwajima’




MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na mgombea Urais kupitia chama hicho, Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka ukweli wake kuhusu namna alivyomteua kada wa chama hicho ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Dkt. Josephat Gwajima kupeperusha bendera ya chama hicho katika jimbo la Kawe.


 


Magufuli amesema hayo leo Ijumaa, Oktoba 9, 2020 wakati akihutubia kwenye kampeni zake zilizofanyika katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.





“Nataka niwaeleze ukweli wana Dar es Salaam, Askofu Gwajima ni mkweli, ni kiongozi mzuri, ndiyo maana hata aliyeongoza kura za maoni Jimbo la Kawe ((Furaha Dominic) ni mtoto wa dada yangu, lakini nililikata jina kwa sababu hawezi kushindana na Gwajima.


 


“Gwajima ni mchapakazi, nichagulieni huyu akalete mabadiliko kwelikweli, Gwajima anasemaga analiamsha dude mpeni kura akaliamshe dude Kawe,”  amesema Magufuli.


 


Katika kura hizo, Furaha Dominick aliongoza kura za maoni za jimbo la Kawe kupitia CCM kwa kujizolea kura 101, akifuatiwa na Angela Kiziga aliyepata kura 85 na nafasi ya tatu ilishikwa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dk. Josephat Gwajima aliyepata kura 79.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad