MISS Tanzania wa mwaka 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K-Lynn’ au ‘Jack Mengi’ ameibuka na kumvaa mnyange mwenzake aliyetwaa taji hilo mwaka 2006, Wema Isaac Sepetu.
K-Lynn amefi kia hatua hiyo, baada ya Wema kushindwa kufi ka kwenye hafla ya mamisi waliowahi kutwaa taji hilo, iliyofanyika wiki iliyopita.
K-Lynn aliandaa hafla hiyo kwenye Hoteli ya Hyyat Regency The Kilimanjaro Hotel iliyopo Posta jijini Dar, iliyokuwa ikiwahusu warembo waliowahi kutwaa taji hilo, kuhamasisha kampeni ya kuwasaidia wanawake na watoto.
Katika hafla hiyo, mamisi kadhaa walihudhuria, akiwemo Millen Magese, Queen Elizabeth Makune, Genevieve Mpangala, Nancy Sumari na wengineo.
Licha ya kujitokeza kwa mamisi hao wengi wa zamani, lakini bado K-Lynn alikumbana na swali la kukosekana kwa mnyange huyo ambaye ni supastaa wa Bongo Movies, Wema.
Akimzungumzia Wema, K-Lynn anasema kuwa, hata yeye anamshangaa mrembo huyo na kujiuliza ni kwa nini hakutokea, pamoja na kwamba alimpa mwaliko kama mamisi wengine.
“Ukweli sijui amekumbwa na nini, maana kama ni mwaliko nimempa kama nilivyowapa wengine,” anasema K-Lynn ambaye kwa muda mrefu hakusikika kwenye ulimwengu wa mastaa, kutokana na kubanwa na majukumu ya kifamilia.
Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilimtafuta Wema ili kujua kulikoni hadi akashindwa kufi ka kwenye hafla hiyo, lakini simu yake iliita bila kupokelewa.