Kagere Mwacheni Nyie! Aweka Rekodi



MSHAMBULIAJI wa Simba raia wa Rwanda, Medie Kagere, ameweka rekodi ya kucheza michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara huku akipachika mabao manne msimu huu wa 2020/21.


Mnyarwanda huyo alianza kwa kusuasua katika ligi kwa kuwekwa benchi na kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji Sven Vandenbroeck katika michezo miwili ya ligi.

Wakati mshambuliaji huyo akianzia benchi, nahodha mkuu wa timu hiyo, John Bocco alikuwa akianza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo akicheza michezo miwili.

Rekodi hiyo ya mabao alianza kwenye mchezo dhidi ya Biashara United uliochezwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam baada ya kufunga bao moja pekee akianza katika kikosi cha kwanza.

Kagere alikuja kufunga bao lingine la pili katika mchezo dhidi ya Gwambina baada ya kupachika bao moja tena kwa mara nyingine katika uwanja huo.Mshambuliaji huyo mwenye uchu wa kufunga mabao alikuja kufunga mabao mengine mawili katika mchezo uliochezwa wikiendi iliyopita ambao walifanikiwa kuwafunga JKT Tanzania mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Bocco yeye alianzishwa katika michezo miwili ya mwanzoni ya ligi na kufunga bao moja pekee walipocheza na Ihefu Uwanja wa Sokoine, Mbeya kabla ya kucheza na Mtibwa Sugar na kutoka bila ya bao.

Kagere mabao yake mawili alifunga kwa vichwa huku mengine mawili akipachika kwa mashuti makali. Kati ya mabao hayo manne aliyofunga mawili alifunga mkoani na mengine Dar.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad