Kesi Ya Mr Kuku Yapigwa Kalenda



Mfanyabiashara,  Tariq Machibya (29) maarufu ‘Mr Kuku’, anaendelea kusota gerezani kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo kutakatisha Sh bilioni 17 kwa kuendesha biashara ya upatu bila leseni.


Kesi hiyo ilikuja jana kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya.


Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai, Upelelezi haujakamilika hivyo aliomba tarehe nyingine ya kutajwa ambapo mahakama iliahirisha kesi na kupanga Oktoba 19 mwaka huu kesi itajwe.

Mr Kuku katika shtaka la kwanza  anadaiwa kusimamia biashara ya upatu.


Inadaiwa  kati ya Januari 2018 na Mei, mwaka huu,  maeneo tofauti Dar ea Salaam alijihusisha na biashara hiyo kwa kukubali na kukusanya fedha kutoka kwa umma kwa kujifanya kwamba watafanya ujasiriamali wa ufugaji kuku na watapata faida asilimia 70 ya mtaji wa awali waliowekeza kwa miezi minne na asilimia 90 ya mtaji huo ya uwekezaji wa miezi sita kiasi ambacho ni kikubwa kibiashara kuliko mtaji uliokusanywa.


Shtaka la pili, anadaiwa kukubali kupokea fedha kutoka kwa umma, katika kipindi hicho anadaiwa kupokea Sh bilioni 17. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad