Kocha Aingia Kudaka Apigwa 7-1

 


Hii ni wiki ya michezo ya kirafiki iliyopo katika kalenda ya FIFA ambapo timu ya taifa ya Ukraine jana ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ufaransa na kupoteza kwa magoli 7-1.


Ufaransa walipata ushindi huo mnono lakini inawezekana hujui kilichopo nyuma ya pazia, wakati mchezo huo unakaribia kuanza magolikipa wa Ukraine wote namba 1 hadi 3 walibaina kuwa na maambukizi ya Corona.




Hivyo Ukraine wakawa hawana kipa na kwakuwa game inabidi ichezwe, basi kocha wao msaidizi ambaye aliwahi kucheza nafasi ya golikipa Oleksandr Shovkovskiy ,45, aliamua kuingia kucheza kama kipa na kujikuta wakipigwa 7-1, Oleksandr amestaafu soka la kimataifa 2012 na ngazi ya club 2016.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad