Kocha wa zamani wa Yanga apata ulaji Kenya



Shirikisho la Soka nchini Kenya limemteua Jacob 'Ghost' Mulee kuwa kocha mkuu mpya wa Harambee Stars.

FKF ikifanya utambulisho wa Jacob Mulee ambaye sasa ndiye kocha mkuu wa Harambee Stars.


Mulee anachukua nafasi ya Francis Kimanzi ambaye aliondoka katika nafasi ya kuinoa Harambee Stars jana baada ya kutangaza kujiuzulu.


Kocha huyo anarejea kikosini baada ya miaka 10 lakini akiwa na sifa ya ushujaa wake wa kuingoza Harambee Stars kwenye kombe la mataifa ya Afrika 2014 ambapo Kenya iliondolewa kwenye hatua ya makundi.


Akizungumza baada ya kusaini mkataba,Mulee amesema "Ni heshima kuwa kocha wa Harambee Stars kwa mara ya pili na kazi iliyo mbele yangu hivi sasa ni kufuzu kwa AFCON ya 2021."


Mulee anatarajiwa kutangaza benchi lake la ufundi kabla ya wiki hii, na jukumu lake la kwanza litakua ni kuikabili Comoro katika mechi mbili zitakazochezwa mwezi ujao ikiwa ni kufuzu fainali za mataifa ya Afrika 2021.


Katika ngazi ya vilabu Mulee amezifundisha Tusker FC ya Kenya, APR ya Rwanda na Yanga ya Tanzania.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad